?>

Papa Francis: Bajeti za fedha za kununulia silaha zitumike kuepusha majanga ya maradhi siku za usoni

Papa Francis: Bajeti za fedha za kununulia silaha zitumike kuepusha majanga ya maradhi siku za usoni

Kiongozi wa Wakristo wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, amesema ni afadhali bajeti kubwa za fedha zinazotumika duniani kwa ajili ya kununulia silaha zitumiwe kuzuia na kupeusha majanga ya dunia nzima ya maradhi katika siku za usoni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Papa Francis ametoa mwito huo katika hafla ya dua maalum ya kila mwezi iliyofanyika katika makao makuu ya kanisa katoliki huko Vatican, mjini Rome na akaomba kwa jaha ya mtakatifu Bibi Maryam (as) dhamiri za wanadamu zipate mtikisiko na kuzinduka ili kiwango kikubwa mno cha fedha kinachotumiwa kuboresha na kuunda silaha za kisasa zaidi duniani, kitumiwe kuinua kiwango kinachohitajika cha mitalaa na utafiti kwa ajili ya kuepusha kutokea masaibu yanayofanana na maradhi ya Covid-19 katika mustakabali.

Kiongozi wa Wakiristo wa Kanisa Katoliki duniani ametoa mwito huo katika hali ambayo, ripoti ya hivi karibuni ya taasisi ya kimataia ya tafiti za amani ya Stockholm imeonyesha kuwa licha ya dunia kukumbwa na janga la virusi vya corona, katika mwaka 2020 gharama za kijeshi za mataifa ya dunia ziliongezeka kwa asilimia 2.6 na kufikia karibu dola trilioni mbili.

Marekani iliongeza bajeti yake ya matumizi ya kijeshi kwa asilimia 4.4 na kufikia dola bilioni 778 na kuwa nchi inayoongoza kwa kutumia kiwango cha juu zaidi cha fedha kwa masuala ya kijeshi. 

Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa, Saudi Arabia inashika nafasi ya kwanza kati ya nchi za Kiarabu na ni ya sita kati ya nchi zote duniani kwa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya bajeti ya masuala ya kijeshi.

Taasisi hiyo ya kimataifa ya tafiti za masuala ya amani ya Stockholm, imebainisha katika ripoti yake hiyo kuwa, mnamo mwaka 2020, Saudia ilikuwa nchi pekee ya Kiarabu, miongoni mwa nchi kumi zilizoongoza duniani kwa bajeti kubwa za masuala ya kijeshi; ikiwa imeshika nafasi ya sita katika uga huo kwa kutanguliwa na nchi tano tu ambazo ni Marekani, China, India, Russia na Uingereza.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*