?>

Pongezi kwa kuadhimisha Sikukuu ya Eid Ghadir Khum

Pongezi kwa kuadhimisha Sikukuu ya Eid Ghadir Khum

Leo Alhamisi tarehe 29 Julai mwaka 2021 inayosadifiana na tarehe 18 Dhul-hija mwaka 1442 Hijria ni Sikukuu ya Idd Sayyid Ghadir Khum, moja ya Idd kubwa za Waislamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ghadir Khum ni eneo lililoko baina ya Makka na Madina ambako Mtume Muhammad (S.A.W) akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija  kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake. 

Siku hiyo Mtume (SAW) alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake. Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui." Mtume SAW pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlubaiti wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*