?>

Qatar: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni ukiukaji wa maazimio ya kimataifa

Qatar: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni ukiukaji wa maazimio ya kimataifa

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imelaani vikali mpango mpya wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa ya serikali ya Qatar imeeleza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya kimataifa.

Sehemu moja ya taarifa hiyo ya Qatar inasema, mipango ya Israel ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni tishio kwa juhudi za kimataifa zenye lengo la kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina kwa kutegemea maazimio ya kimataifa.

Tamko hilo la Qatar limekuja baada ya utawala wa Kizayuni kutangaza kuwa, unapanga kupitisha mpango wa kujenga nyumba mpya zipatazo elfu nne katika eneo la Ufukwe wa Magharibi, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Shirika la ujenzi la utawala wa muda wa Kizayuni katika Ufukwe wa Magharibi limetangaza kuwa, kamati ndogo ya ujenzi wa vitongozi iliyo chini ya baraza kuu la mipango la Tel Aviv imepanga kuanzisha ujenzi wa nyumba mpya zipatazo 3,988 kwa ajili ya walowezi wa Kizayuni.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*