?>

Raeisi: Kulinda haki za wanadamu ni msingi wa siasa za Jamhuri ya Kiislamu

Raeisi: Kulinda haki za wanadamu ni msingi wa siasa za Jamhuri ya Kiislamu

Rais mteule wa Iran amesema kuwa, kulinda haki za wanadamu ndiyo msingi wa siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Ibrahim Raeisi aliyasema hayo alasiri ya jana katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin. Sambamba na kutoa mkono wa Idul Haj kwa Waislamu wote, Sayyid Raeisi ameitaja idi hiyo kuwa ni sikukuu kubwa ya Waislamu na kuongeza kuwa: Kwa mujibu wa dini zote zinazofuata mafundisho ya Nabii Ibrahim (as), Iran na Vatican zinapaswa kuwa bega kwa bega na mataifa yote yanayodhulumiwa duniani na kupambana na madola ya kidhalimu. 

Rais mteule wa Iran ametilia mkazo umuhimu wa kuwepo mazungumzo baina ya dini zote za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuanzisha amani endelevu kote duniani na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama serikali inayoongozwa kwa mfumo wa demokrasia ya kidini, inakaribisha mazungumzo na ushirikiano baina ya dini zote za mbinguni hususan Ukristo. 

Sayyid Raeisi amesema: "Siasa za Jamhuri ya Kiislamu za kuwatetea watu wa Palestina, kupambana na utawala ghasibu na vamizi wa Israel, kuwalinda na kuwatetea watu wa Yemen, kupambana na ugaidi wa makundi ya kitakfiri katika nchi za Iraq na Syria na kuwalinda wafuasi wa dini ya Ukristo nchini Iraq zina msingi katika itikadi zetu ya kidini zinazohimiza udharura wa kulindwa haki za wanadamu." 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin amempongeza Sayyid Ibrahim Raeisi kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Iran na kumtakia mafanikio katika nafasi hiyo. Amesema kuwa, hii leo Tehran na Vatican zina jukumu muhimu la kuimarisha amani na utulivu kote duniani na kushirikiana zaidi kwa ajili ya lengo hilo.      

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*