?>

Rais kizee wa Marekani ala mweleka tena, mara hii ni kutoka juu ya baskeli

Rais kizee wa Marekani ala mweleka tena, mara hii ni kutoka juu ya baskeli

Joe Biden, rais kizee wa Marekani mwenye umri wa miaka 79, kwa mara nyingine amekula mweleka na mara hii ni kwenye baskeli. Mkasa huo umemkuta kwenye jimbo la Delaware tena mbele ya kadamnasi ya watu ambao walikuwa wanasubiri kumsalimia.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Biden, rais kizee wa Marekani alikuwa ameandamana na mkewe, Jill Biden kuendesha baskeli wakati wa asubuhi katika bustani ya  Cape Henlopen karibu na nyumba yao ya ufukweni wakati alipokumbwa na mkasa huo.

Wakati Biden alipoona wafuasi wake, aliamua kufanya pozi za kwenda kuonana nao na kujaribu kuwaonesha kuwa bado nguvu zimo mwilini. Wafuasi wake walianza kumshangiria kila alivyokuwa anawakaribia, lakini wakati alipojaribu kushuka kwenye baskeli alishindwa kujizuia na alikula mweleka hadi chini.

Baada ya askari kanzu kumkimbilia haraka na kumuokota alipoanguka, Biden aliwaambia waandishi wa habari: "Mimi ni mzima. Mguu wangu tu ulikwama kwenye pedali ya baskeli."

Vituko kama hivyo ni jambo la kawaida kwa rais huyo kizee wa Marekani kuanzia kwenye maneno mpaka kwenye vitendo. 

Tarehe 19 Machi 2021, Biden alikula mweleka mara tatu mfululizo wakati alipokuwa anapanda ngazi za ndege kuelekea Atlanta kwa ajili ya kushiriki kikao cha viongozi wa jumuiya ya Waasia waishio Marekani.

Hivi sasa familia ya Biden iko kwenye mapumziko marefu katika nyumba yao ya ufukweni karibu na bustani ya Cape Henlopen katika jimbo la Delaware. Juzi Ijumaa, Biden na mkewe Jill Biden walisherehekea mwaka wa 45 wa ndoa yao.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*