?>

Rais Rouhani ataka kuimarishwa ushirikiano na Nigeria katika nyanja za kimataifa

Rais Rouhani ataka kuimarishwa ushirikiano na Nigeria katika nyanja za kimataifa

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kuimarishwa zaidi ushirikiano wa Tehran na Abuja.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Hassan Rouhani ameyasema hayo wakati wa kupokea hati za utambulisho za balozi mpya wa Nigeria mjini Tehran. Amesema kuwa, nchi mbili hizi zina uwezo mkubwa katika nyanja za biashara, kilimo, sayansi na teknolojia hususan katika sekta ya nishati. 

Rais Rouhani ameongeza kuwa, uwezo huo unapaswa kutumiwa ipasavyo kwa ajili ya maslahi ya mataifa ya nchi hizo mbili. 

Vilevile ameashiria umuhimu wa kustawishwa uhusiano wa Tehran na Abuja na kusema anatarajia kuwa, uhusiano wa miaka mingi wa nchi hizo mbili utaimarishwa zaidi kwa kutumiwa uwezo na ushirikiano wao. Vilevile ameashiria ushirikiano wa Iran na Nigeria katika jumuiya za kimataifa na kusema kuwa, ushirikiano huo unaweza kuimarisha zaidi uhusiano wa pande mbili katika masuala mbalimbali.

Kwa upande wake balozi mpya wa Nigeria mjini Tehran, amesisitiza hamu ya nchi yake ya kuboresha zaidi uhusiano na Iran na kusema Abuja ina azma ya kustawisha zaidi mahusiano ya pande mbili.

Balozi Suleiman amesema Nigeria inaweza kuwa soko kubwa kwa bidhaa za Iran na kuongeza kuwa, kuwepo kwa makampuni ya Jamhuri ya Kiislamu katika nchi hiyo ya Kiafrika kunaweza kutoa msaada mkubwa katika ustawi wa Nigeria.      

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*