?>

Rais wa DRC aamuru wanajeshi na polisi kuchukua jukumu la kuendesha mzingiro katika majimbo ya kaskazini

Rais wa DRC aamuru wanajeshi na polisi kuchukua jukumu la kuendesha mzingiro katika majimbo ya kaskazini

Rais Felix Tchisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametoa amri kwa jeshi na polisi wa nchi hiyo kuchukua jukumu la kuendesha mzingiro katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyio yaliyokumbwa na machafuko na mauaji ya mara kwa mara ya magenge ya waasi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Tchisekedi amesema, wakuu wote wa kiraia wa mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini watakabidhi nafasi zao kwa maafisa wa jeshi la ulinzi au kwa maafisa wa Jeshi la Polisi Taifa. Uamuzi huo utaanza kutekeleza keshokutwa Alkhamisi na utadumu kwa takriban siku 30.

Ijumaa iliyopita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza 'hali ya mzingiro' katika mikoa hiyo miwili inayoshuhudia mapigano na umwagaji damu kwa miezi kadhaa sasa.

Msemaji wa serikali, Patric Muyaya amesema, Rais Tchisekedi amefikia uamuzi huo baada ya kushauriana na Waziri Mkuu Lukonde Sama pamoja na mabaraza ya Sanate na Bunge.

Licha ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutangaza mzingiro wa mikoa hiyo ya Ituri na Kivu Kaskazini, lakini mauaji ya raia yameendelea. 

Siku chache zilizopita, genge moja lenye silaha liliua takriban watu 19 wakiwemo wanajeshi 10  wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kushambulia vijiji viwili mashariki mwa nchi hiyo.

Ongezeko la mashambulizi ya magenge yenye silaha na machafuko ya kikabila yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 300 tangu mwanzoni mwa mwaka huu huku wanajeshi wa serikali na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakijaribu kuleta utulivu mashariki mwa nchi hiyo bila mafanikio. Mauaji hayo ya hivi karibuni yametokea Beni, makao makuu ya Kivu Kaskazini licha ya serikali kutangaza kulizingira jimbo hilo.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Aprili, wakazi wa miji ya Beni na Butembo huko Kivu Kaskazini wamekuwa wakiandamana kulaani mauaji ya waasi wa ADF.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*