?>

Raisi: Iran na Turkmenistan zina uhusiano uliokita mizizi

Raisi: Iran na Turkmenistan zina uhusiano uliokita mizizi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uhusiano wa pande mbili wa nchi hii na Turkmenistan ni wa kidugu na uliokita mizizi.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Rais Ebrahim Raisi amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika kikao na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Turkmenistan, Serdar Berdimohamedow na kuongeza kuwa, taifa hili lina hamu ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa miaka 20 na jirani yake huyo.

Sayyid Raisi amesema uhusiano wa nchi mbili hizi ni mzuri na umeimarika zaidi katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, na kwamba katika safari yake mjini Ashgabat miezi michache iliyopita walifikia makubaliano juu ya kuimarisha ushirikiano katika nyuga za uchukuzi na ubadilshanaji wa gesi.

Rais wa Iran amesema hakuna kizuizi cha kuyafanya mataifa haya mawili yasipige jeki uhusiano wao katika nyuga za biashara, uchumi, maji, na nishati. 

Kadhalika amempongeza aliyekuwa rais wa Turkmenistan, Gurbanguly Berdimuhamedow kwa jitihada zake za kuboresha uhusiano wa Tehran na Ashgabat, na kueleza kuwa anatumai mwana wa kiume wa rais huyo atafuata nyayo hizo katika uongozi wake.

Kwa upande wake, Rais Serdar Berdimohamedow wa Turkmenistan mbali na kusisitizia haja ya kupanuliwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa nchi mbili hizi, amesema nchi yake itafaya kila iwezalo kuhakikisha kuwa ushirikiano wa mataifa haya katika nyuga za nishati na usafiri unaimarishwa zaidi. 

Kabla ya kuhutubia waandishi wa habari, marais hao wawili walishiriki hafla ya kusainiwa mikataba tisa ya maelewano baina ya mataifa haya mawili katika nyuga mbalimbali kama uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, utamaduni, mawasiliano, usalama na nishati.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*