?>

Raisi: Kuna udharura kwa jamii ya mwanadamu hii leo kumtilia maanani Mwenyezi Mungu na umaanawi

Raisi: Kuna udharura kwa jamii ya mwanadamu hii leo kumtilia maanani Mwenyezi Mungu na umaanawi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa mazingatio kwa Mola Muumba na suala la umanaawi ni jambo la udharura mkubwa hii leo kwa jamii ya mwanadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Sayyid Ebrahim Raisi amesisitiza leo Jumanne wakati akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Andeji Yusovic Balozi Mpya wa Vatican hapa Tehran kwamba, ni jambo la dharura hii leo kwa jamii ya mwanadamu kutoa mazingatio kwa Mola Muumba na suala la umaanawi; na kwamba kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani ni nukta zinazotukutanisha pamoja dini za mbinguni ambazo zinaagiza kuwepo umoja na mshikamano kati yetu.

Ameongeza kuwa wale wanaodhulumu na kufanya ukandamizaji duniani hii leo kama wangezingatia mafundisho ya Nabii Isa Masih (a.s) wasingeweza kutenda dhulma hizo; na Vatican inaweza kuwa na nafasi na mchango muhimu katika uwanja huo.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, mafundisho ya dini ya Ukristo na kile alichotufunza Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w) yanapasa kujadiliwa katika vikao vya kielimu ili kukurubisha zaidi mitazamo baina yetu.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*