?>

Raisi: Uhusiano mzuri wa Iran na Oman utaongeza ushirikiano wa kikanda

Raisi: Uhusiano mzuri wa Iran na Oman utaongeza ushirikiano wa kikanda

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, misimamo ya Iran na Oman katika masuala mengi inakaribiana sana na akaongeza kuwa, uhusiano mzuri wa nchi hizo mbili utaongeza ushirikiano wa kikanda.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo alifajiri ya kuamkia leo alipowasili hapa mjini Tehran akitokea Oman ambako aliongoza ujumbe wa ngazi za juu katika ziara ya siku moja aliyofanya kwa mwaliko wa Sultan Haitham bin Tariq Al Said wa nchi hiyo.

Kukutana na kuzungumza na Sultan wa Oman, Naibu Waziri Mkuu, wafanyabiashara na wadau wa kiuchumi pamoja na Wairan wanaoishi Oman zilikuwa miongoni mwa ratiba za ziara hiyo ya Rais Raisi.

Katika ziara hiyo, maafisa wa pande mbili za Tehran na Muscat walisaini hati 12 za ushirikiano katika nyuga za nishati, siasa, uchukuzi na usafirishaji, mashirikiano ya kidiplomasia, mahusiano ya kibiashara, kiuchumi na kielimu, hifadhi ya mazingira na michezo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Mehr Abad mara baada ya kuwasii nchini, Rais Raisi amebainisiha kuwa, katika vikao alivyofanya jana Jumatatu na viongozi wa ngazi za juu wa Oman imesisitizwa kuwa, kuna ulazima wa nchi mbili kushirikiana kimataifa na kwamba misimamo ya nchi mbili katika masuala mengi inalingana na kukaribiana sana.

Sayyid Ebrahim Raisi ameendelea kueleza kwamba, katika kikao na wadau wa kiuchumi, biashara na masoko wa nchi mbili, yalijadiliwa matatizo ya wadau hao katika masuala ya biashara, uhamishaji fedha na masuala ya kifedha, kibenki na forodha mbele ya waziri wa viwanda, madini na biashara wa Iran na waziri wa biashara wa Oman na kwamba karibuni hivi vizuizi vilivyopo vitaondolewa ili kufungua njia kwa biashara na shughuli za kiuchumi.

Rais wa Iran amefafanua pia kuwa wafanyabishara wa Oman na pia wa Iran wana uelewa mdogo kuhusu uwezo na fursa zilizopo katika nchi mbili, kwa hivyo imeonekana kuna haja ya kuanzishwa ofisi ya kibiashara ya Iran nchini Oman na ikaamuliwa kwamba ofisi hiyo ianzishwe haraka iwezekanavyo ili kuwatambulisha wadau wa kiuchumi uwezo na fursa zinazopatikana katika nchi mbili hizi.../ 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*