?>

Ramaphosa: Ghasia za sasa Afrika Kusini ni mbaya zaidi

Ramaphosa: Ghasia za sasa Afrika Kusini ni mbaya zaidi

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema ghasia zilizosababisha mauaji nchini humo hazijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi. Machafuko hayo yamesababishwa na maandamano ya wiki nzima ya kupinga hatua ya rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kufungwa miezi 15 gerezani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Machafuko hayo yamesababishwa na maandamano ya wiki nzima ya kupinga hatua ya rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kufungwa miezi 15 gerezani. Akilihutubia taifa jana usiku, Ramaphosa amesema baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini yamekabiliwa na siku kadhaa za vurugu, uharibifu wa mali na uporaji ambao haujawahi kutokea katika historia ya demokrasia ya nchi hiyo. Ramaphosa amesema ghasia hizo zimevuruga mpango wa kutoa chanjo ya virusi vya corona na kwamba zitazidisha umasikini, kukosekana kwa ajira na watu kupoteza maisha. Watu 10 wameuawa, wengine wakiwa na majeraha ya risasi waliyopata baada ya jeshi kupelekwa kwenye maeneo kadhaa ya nchi. Watu 489 wamekamatwa. Ramaphosa amesema aliamuru jeshi lipelekwe kuwasaidia polisi kukabiliana na waandamanaji.

Katika mandamano kama hayo ya siku kadhaa zilizopita, wafusi wa Zuma walichoma moto magari na maeneo ya umma huko KwaZulu Natal. 

Wiki iliyopita Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini iliagiza Zuma afungwe jela kwa kukataa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa ufisadi uliofanyika katika kipindi chake cha uongozi kutoka 2009 hadi 2018. 

Zuma, 79, anakanusha kuhusika na ufisadi na amesema kuwa ni mhanga wa njama za kisiasa.

Rais mstaafu wa Afrika kusini Jacob Zuma, alijikabidhi kwa polisi siku kadhaa zilizopita na kupelekwa katika gereza lililo karibu na nyumbani kwake katika jimbo la KwaZulu Natal.

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alilazimika kujiuzulu mwezi Februari mwaka 2018 kutokana na mashinikizo ya chama tawala cha ANC.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*