?>

Redio ya China: Marekani ndiyo inayofanya chokochoko dhidi ya Iran katika Ghuba ya Uajemi

Redio ya China: Marekani ndiyo inayofanya chokochoko dhidi ya Iran katika Ghuba ya Uajemi

Redio ya serikali na kimataifa ya China imeashiria harakati za jeshi la Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kueleza kwamba, kinyume na madai ya Washington, Marekani ndiyo inayoendelea kufanya chokochoko hivi sasa dhidi ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Redio hiyo ya China imeashiria rekodi ya vitendo vya chokochoko ambavyo jeshi la Marekani limekuwa likifanya katika Ghuba ya Uajemi na eneo hususan dhidi ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubainisha kuwa, jeshi la Marekani limetuma manowari zake Ghuba ya Uajemi umbali wa kilomita elfu 10 kutoka ardhi ya nchi hiyo na kuzipitisha kwenye lango bahari la Hormuz ambalo ni mithili ya ua wa nyumba ya Wairani huku zikianzisha makabiliano na boti za ulinzi za Iran.

Redio hiyo imekumbusha kuwa, hivi karibuni, Marekani imetuma hata nyambizi yake ya nyuklia katika Ghuba ya Uajemi ambayo ni silaha hatari zaidi ya kivita kuliko hata manowari inayobeba ndege za kivita na ikaongeza kuwa, Wairan wanayo haki ya kupinga kuwepo kijeshi Marekani na kuichukulia hatua hiyo kuwa ni kizuizi kwa amani na uthabiti wa eneo.

Kwa mujibu wa redio ya serikali na kimataifa ya China, kama ilivyo nchini Afghanistan, ambako wananchi wengi wanaitakidi kuwa kuwepo jeshi la Marekani ni kikwazo cha kufikiwa mapatano ya kitaifa nchini mwao, katika eneo la Ghuba ya Uajemi pia Marekani inaonekana ni kizuizi cha kumalizika mivutano iliyopo; na hakuna shaka kwamba, kuwepo kwake kijeshi, ikiwa ni nchi ajinabi na ya nje ya eneo, si kwa ajili ya kulinda amani na uthabiti wa Ghuba ya Uajemi.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*