?>

Ripoti: Janga la Covid-19 lilivyoathiri uchumi wa mataifa ya Afrika

Ripoti: Janga la Covid-19 lilivyoathiri uchumi wa mataifa ya Afrika

Licha ya kuwa, bara la Afrika halijashuhudia maambukizi makubwa na maafa yanayotokana na janga la Covid-19, lakini mataifa mengi katika bara hilo, yameendelea kushuhudia kuyumba kwa uchumi wao kutokana na kuendelea kuongezeka kwa virusi hivyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Baada ya kuzuka kwa maambukizi hayo mapema mwaka huu, Shirika la Fedha Duniani IMF lilitangaza kuwa, uchumi wa bara la Afrika, ungeshuka kwa asilimia tatu, lakini utakua kwa asilimlia 3.1 mwaka ujao wa 2021 unaoanza kesho.

Ripoti ya IMF inaonyesha kuwa, uchumi katika nchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania umeyumba lakini umekuwa ukionesha dalili za kuimarika.

Mataifa yenye utajiri wa mafuta barani Afrika kama Algeria, Angola na Nigeria, yameathirika pakubwa kufuatia kushuka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia.

Nchi ya Afrika Kusini, taifa la pili kwa ukubwa wa uchumi barani Afrika, ndilo lililoathirika zaidi kwa sababu lilianza kupitia hali ngumu ya kiuchumi hata kabla ya kuzuka kwa maambukizi ya Corona na wiki hii, nchi hiyo iliripoti kwamba, kesi za za maambukizo ya virusi hivyo zimepindukia milioni moja; na hivyo kuwa nchi yenye iliyoathiriwa zaidi na Covid-19 barani Afrika.

Morocco ilitoko kaskazini mwa Afrika ndio nchi ya pili barani Afrika kwa kuathirika zaidi na virusi vya Corona ambapo hadi hadi sasa ikifuatiwa na Tunisia.

Aidha kwa upande wa Afrika Mashariki nchi ya Kenya ndio iliyoathiriwa zaidi na maambukizo ya virusi vya Corona ambapo hadi sasa karibu kesi laki moja za maambukizo ya Covid-19 zimesajiliwa nchini humo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni