?>

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA -

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA -

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Kazakhstan zimekuwa na uhusianio mzuri kwa miaka 30 iliyopita lakini uhusiano huu hautoshi.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo katika mkutano wa waandishi wa habari akiwa pamoja na mgeni wake, Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Kemelevich Tokayev. Amesema kuwa, Iran na Kazakhstan zinaweza kuboresha zaidi uhusiano wao na kuongeza kuwa, mikataba iliyosainiwa leo au siku za nyuma ni ishara muhimu ya nia ya nchi hizo mbili ya kuendeleza uhusiano.

Rais Ebrahim Raisi amesema, "Uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 katika miezi ya hivi karibuni, na kiwango cha mahusiano haya kinaweza kuongezeka zaidi; katika hatua ya kwanza tunaweza kuongeza kiwango cha biashara kati ya pande mbili hadi dola bilioni 3 kwa mwaka.

Amesema: "Mbali na uhusiano wa pande mbili, tumedhamiria kupanua uhusiano wa kikanda baina ya nchi hizo mbili. Kwa mfano, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika mashirika ya kikanda kama vile Shirika la Ushirikiano la Shanghai na Umoja wa Eurasia unaweza kuimarishwa zaidi."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameashiria hali ya Afghanistan na kusema: "Tuna maoni ya pamoja kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa. Kwa mfano, tunaafikiana juu ya Afghanistan na haja ya kuundwa serikali jumuishi nchini humo." Amesisitiza pia kwamba Iran na Kazakhstan zinaafikia kwamba uwepo wa wageni katika ukanda huu hauleti usalama na badala yake utasababisha matatizo mengi.
Wakati huo huo hati 9 za maelewano na waraka wa ushirikiano zimetiwa saini mjini Tehran katika hafla iliyohudhuriwa na Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kazakhstan.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*