?>

Rouhani: Iran ina uwezo wa kurutubisha urani hadi kiwango cha asilimia 90

Rouhani: Iran ina uwezo wa kurutubisha urani hadi kiwango cha asilimia 90

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria historia ya kuidhinishwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema: "Sekta yetu ya nyuklia imebaki kuwa yenye nguvu na hilo limedhihirika zaidi katika miezi ya hivi karibuni."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo katika kikao cha baraza la mawaziri na kuongeza kuwa: "Tawala za Israel na Saudia Arabia pamoja na wenye misimamo mikali Marekani na  walio dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu tokea mwanzo walikuwa wanapinga mapatano ya JCPOA na daima wamekuwa wakitaka kuyavuruga." Akiashiria kuja Trump madarakani na kujiondoa katika JCPOA Rouhani amesema: wapinzani wa JCPOA walimpata "mtu mjinga na kisha wakamshawishi ajiondoe katika JCPOA ili mapatano hayo yasambaratike." Rais Rouhani amesema wapinzani hao wa JCPOA walikuwa wamemfahamisha Trump kuwa iwapo atajiondoa katika JCPOA basi katika kipindi cha masaa 24 Iran nayo itajiondoa na dunia nzima itasema Iran ndiyo iliyosambaratisha mapatano hayo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, maadui walikosea katika mahesabu yao kwani hawakufikia malengo waliyokusudia. Amesema lengo lao kuu lilikuwa ni kuuangusha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kusambaratisha uchumi wa Iran lakini walifeli.

Rouhani ameongeza kuwa, katika mapatano ya JCPOA, sekta ya nyuklia ya Iran imeweza kubakia ikiwa na nguvu na sasa Shirika la Atomiki la Iran linaweza kurutubisha madini ya urani hadi kiwango cha asilimia 90 bila tatizo lolote. Halikadhalika amesisitiza kuwa, shughuli zote za nyuklia za Iran zinafanyika kwa malengo ya amani.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*