?>

Rouhani: Vikwazo dhidi ya Iran havikuwa na faida kwa maadui

Rouhani: Vikwazo dhidi ya Iran havikuwa na faida kwa maadui

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havina faida kwa maadui na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imevuka vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani ambaye hii leo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Tehran amesema vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havikuzaa matunda yaliyotarajiwa na maadui na kuongeza kuwa, lengo kuu la mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani dhidi ya serikali na taifa la Iran ni kuburuta Jamhuri ya Kiislamu kwenye meza ya mazungumzo lakini kamwe suala hilo hilo halitatatimia.

Kuhusu mpango wa Amani ya Hormuz, Rais Rouhani amesema: Ni wazi kwa walimwengu wote kwamba, eneo la magharibi mwa Asia haliwezi kupata amani na utulivu bila ya kushirikishwa Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia nafasi na mchango wa shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo la magharibi mwa Asia na kusema: Shahidi Soleimani alikuwa akifanya juhudi za kuimarisha amani katika eneo nyeti na muhimu la Ghuba ya Uajemi na magharibi mwa Asia.

Rouhani pia ameashiria mgogoro wa Yemen na kusema: Saudi Arabia inapaswa kukomesha kabisa uvamizi na mshambulizi yake dhidi ya nchi hiyo, na masuala ya Yemene wanapaswa kuachiwa Wayemeni wenyewe. 

.............
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni