?>

Russia: Lebanon haipasi kufanywa mahali pa kukomoana na kulipiziana visasi nchi zingine

Russia: Lebanon haipasi kufanywa mahali pa kukomoana na kulipiziana visasi nchi zingine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema, ana matumaini serikali mpya ya Lebanon itaweza kuhitimisha mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa na akataka nchi hiyo isitumiwe kuwa mahali pa nchi zingine kukomoana na kulipiziana visasi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Lavrov ameyasema hayo mjini Moscow katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya pamoja na mgeni wake waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia ameeleza kwamba, wajihusishaji wa kisiasa wa nje wanajaribu kuingilia masuala ya ndani ya Lebanon na akaongeza kwamba kwa mtazamo wa Moscow hatua za aina hiyo ni haribifu kwa Lebanon yenyewe na kwa hali ya eneo.

Watalaamu wa siasa za eneo wanasema, Marekani na Saudi Arabia zinaingilia masuala ya ndani ya Lebanon na kujaribu kubadilisha mkondo wa mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo.

Lavrov ameendelea kueleza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, yeye na waziri mwenzake wa Lebanon wamezungumzia pia shughuli za mashirika ya Russian Oil na Novotank kwa ajili ya kustawisha sekta ya nishati ya Lebanon.

Mapema kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi mbili, wizara ya mambo ya nje ya Russia ilieleza katika taarifa kwamba, Moscow daima imekuwa ikisisitizia kuheshimiwa mamlaka ya utawala, uhuru na umoja wa ardhi yote ya Lebanon na inaiunga mkono serikali mpya ya Beirut katika juhudi zake za kuitoa nchi hiyo kwenye lindi la mgogoro.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, uhusiano wa Russia na Lebanon tokea tangu na tangu ni wa kirafiki na ikaongeza kwamba, kustawishwa uhusiano wa pande mbili kunarahisisha kwa mawasiliano ya mpangilio yanayofanywa na Moscow na pande husika katika miundo ya kiserikali ya Lebanon na mirengo athirifu ya kisiasa ya nchi hiyo.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*