?>

Russia yaitahadharisha Marekani kuhusu kuweka makombora ya Hypersonic huko Ulaya

Russia yaitahadharisha Marekani kuhusu kuweka makombora ya Hypersonic huko Ulaya

Ubalozi wa Russia mjini Washington umetahadharisha juu ya mpango wa Marekani wa kutaka kuweka makombora yenye kasi kubwa kuliko sauti (hypersonic missile) katika nchi za Ulaya na kusema hatua hiyo itaibua mapigano yasiyo ya lazima.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ubalozi wa Russia mjini Washington leo umetoa taarifa na hapa ninanukuu: Sisi tumeikumbusha Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kwamba kitendo cha kutuma kivyovyote vile makombora ya hypersonic katika nchi za Ulaya kinatatiza pakubwa amani.'

Taarifa ya ubalozi wa Russia mjini Washington imeongeza kuwa, muda mfupi wa kurushwa makombora hayo kutatoa muda mdogo kwa Russia kuchukua maamuzi; jambo ambalo huenda likazidisha mapigano yasiyo ya lazima.  

John Kirby Msemaji wa Pentagon hivi karibuni alisema katika mkutano na waandishi wa habari akijibu jaribio la makombora hayo ya Hypersonic lililofanywa na Russia kuwa, makombora hayo mapya ya Russia kuna uwezekano mkubwa yakavuruga amani na uthabiti kwa sababu yanawea kubeba pia vichwa vya nyuklia, na hivyo makombora hayo kuzidi kuwa hatari. 

Waziri wa Ulinzi wa Russia Jumatatu wiki hii aliarifu kuwa nchi hiyo imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lake la Hyepersonic kuanzia bahari Nyeupe kuelekea bahari ya Barent. Kombora hilo linakadiriwa kuwa na kasi ya kwenda zaidi ya sauti kwa kipimo cha Mach 7 katika umbali wa zaidi ya kilomita 350. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*