?>

Russia yasema imeharibu silaha ambazo Ukraine ilipokea kutoka Marekani, Ulaya

Russia yasema imeharibu silaha ambazo Ukraine ilipokea kutoka Marekani, Ulaya

Wizara ya Ulinzi ya Russia inasema imefanikiwa kuharibu idadi kubwa ya silaha na zana za kivita ambazo Ukraine imepokea kutoka Marekani na Ulaya.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa ya Jumamosi ya wizara hiyo imesema silaha hizo zilikuwa katika maeneo ya Ukraine ya Kharkiv na bandari ya Odesa.

Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zimekuwa zikiipa serikali ya Ukraine idadi kubwa ya silaha zinazotumika kukabilia na jeshi la Russia.

Huku vita vya Ukraine vikiwa vinaingia siku yake ya 74 mkuu wa kamandi ya Majeshi ya Ufaransa Jenerali Thierry Burkhard amesema nchi za Magharibi zinapaswa kujitayarishwa kwa uhasama wa muda mrefu na Russia. Amesema nchi za Ulaya sasa zinapaswa kujizatiti zaidi kwa silaha na kuimarisha umoja kwa ajili ya mashindano ya muda mrefu na Russia.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema, vikwazo vya Magharibi havina athari yoyote mbele ya irada ya watu wa nchi hiyo.

Baada ya Russia kuanzisha operesheni ya kijeshi ndani ya ardhi ya Ukraine mnamo tarehe 24 Februari 2022, Marekani na nchi zingine za Magharibi zilianza kuiwekea Moscow vikwazo vikubwa vya kiuchumi, kama hatua ya kukabiliana na mashambulio ya kijeshi ya nchi hiyo dhidi ya Ukraine.

Vikwazo hivyo vimewekwa huku Magharibi ikiwa inachelea kuwa kushadidisha vikwazo dhidi ya Russia katika sekta ya uchumi hasa mafuta na gesi kutaathiri na kuvuruga zaidi hali ya uchumi ya Ulaya na masoko ya nishati duniani.

Vikwazo mbalimbali ilivyowekewa Russia hadi sasa vimeibua changamoto nyingi kwa uchumi wa nchi za Ulaya.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*