?>

Russia yatayarisha rasimu ya azimio la kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria

Russia yatayarisha rasimu ya azimio la kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria

Duru za habari zimeripoti kuwa, Russia imetayarisha rasimu ya azimio dhidi ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Isarel huko Syria kwa ajili ya kuwasilishwa kwwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tarehe 10 mwezi huu wa Juni utawala wa Kizayuni wa Israel ulirusha makombora kadhaa kutoka Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na kupiga baadhi ya maeneo ya Damascus ukiwemo uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji huo.

Shambulizi la Israel kwenye uwanja wa ndege wa Damascus lilijeruhi raia mmoja na kusababisha uharibifu wa mali.

Rasimu hiyo iliyoandaliwa na Russia inasema: “Shambulio hili lilitekelezwa kwa njia ambayo inakiuka sheria za kimataifa na mamlaka ya Syria na kudhoofisha amani ya nchi hiyo, na kwa sababu hiyo, wahusika wa shambulio hili lazima wawajibishwe."

Shambulio hilo limepingwa vikali na serikali ya Moscow, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilimwita na kumsaili balozi wa Israel mjini Moscow kufuatia uchokozi huo.

Wakati huo huo, Faisal Miqdad Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema katika kikao cha pamoja cha kamati ya Syria na Russia kilicholenga kuwarejesha makwao wakimbizi wa Syria kwamba vita na uharibifu unaoshuhudiwa nchini Syria unatokana na uungaji mkono na misaada ya nchi za Magharibi kwa makundi ya kigaidi yenye silaha.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*