?>

Salamu za rambirambi za Papa Francis kwa watu wa Iraq kufuatia ajali ya moto

Salamu za rambirambi za Papa Francis kwa watu wa Iraq kufuatia ajali ya moto

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, ambalo linajulikana pia kama Kanisa Katoliki la Roma, amewatumia salamu za rambirambi wahanga wa ajali ya moto ambayo imetokea karibuni katika Hospitali ya al-Hussein nchini Iraq.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya makao makuu ya Papa Francis huko Vatican, katika ujumbe wake wa rambirambi kwa wahanga wa ajali hiyo ya moto, Papa ameeleza kusikitishwa kwake na tukio hilo la moto uliozuka katika kitengo kinachowahudumia wagonjwa wa corona katika Hospitali ya al-Hussein at-Ta'limi, iliyoko katika mji wa Nassiriya katika mkoa wa Dhi Qar nchini Iraq na kuzitakia subira na utulivu familia za wahanga wa ajali hiyo chungu.

Sehemu ya ujumbe wake huo inasema kwamba pamoja na kutokea ajali hiyo lakini wagonjwa, wafanyakazi na wakuu wa hospitali hiyo wanapasa kutambua na kushukuru neema nyingine nyingi za Mwenyezi Mungu na kufarijika na neema hizo.

Vyombo vya Iraq vimetangaza kwamba moto huo uliozuka hospitalini hapo jana alfajiri umepelekea watu 108 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Huo ni moto wa pili kutokea hospitalini huko Iraq katika kipindi cha masaa machache yaliyopita. Moto mwingine uliozuka karibuni katika gorofa ya nne ya Wizara ya Afya ya Iraq umeteketeza nyaraka zote muhimu za wizara hiyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*