?>

Sayyid Nasrullah: Utawala wa kibaguzi wa Israel utaangamia

Sayyid Nasrullah: Utawala wa kibaguzi wa Israel utaangamia

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika na kuangamia na kwamba matukio yote yanayoshuhudiwa hivi sasa katika eneo la Asia Magharibi yapo dhidi ya maslahi ya utawala huo pandikizi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Hassan Nasrullah alisema hayo jana Jumanne katika mahojiano na Radio Noor ya Lebanon, kwa mnasaba wa kutimia miaka 20 tangu kukombolewa eneo la kusini mwa Lebanon toka kwenye makucha ya Wazayuni na kueleza bayana kuwa: hakuna shaka kuwa utawala wa Israel utasambaratika.

Huku akiutaja utawala huo kama saratani, Sayyid Nasrullah ameonya kuhusu njama za Tel Aviv za kuunda 'taifa la Palestina' nchini Jordan akisisitiza kuwa, mpango huo unakusudia kupora ardhi zote za Wapalestina.

Kadhalika Sayyid Nasrullah sambamba na kuashiria kuhusu mpango wa kibaguzi wa "Muamala wa Karne" amelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kupora na kuteka ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Aidha Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameeleza bayana kuwa: Uwepo majeshi ya Marekani katika eneo unaashiria wazi udhaifu wa waitifaki wa Washington na nguvu kubwa ya mrengo wa muqawama.

Itakumbukuwa kuwa, tarehe 25 Mei 2000, utawala wa Kizayuni licha ya kuwa na nguvu za kijeshi, ulisalimu amri mbele ya wanamapambano wa Kiislamu wa Lebanon na ulilazimika kukimbia kwa madhila kusini mwa nchi hiyo. Kila mwaka wananchi wa Lebanon wanaadhimisha siku hiyo ya kukimbia wanajeshi wa mwisho wa Israel kusini mwa nchi yao na siku hiyo wanaiita "Siku ya Muqawama na Ushindi."
Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni