?>

Seneti ya Pakistan yapasisha azimio dhidi ya njama ya Trump ya "Muamala wa Karne"

Seneti ya Pakistan yapasisha azimio dhidi ya njama ya Trump ya

Baraza la Seneti la Pakistan limepasisha kwa sauti moja azimio linalopinga mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Palestina uliopewa jina la "Muamala wa Karne" likisema kuwa unawataka Wapalestina wasalimu amri kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

(ABNA24.com) Wawakilishi wote 104 wa Baraza la Seneti la Pakistan wamepasisha muswada huo ambao ulipendekezwa na seneta Mushtaq Ahmad Khan wa chama cha Jamaat-e-Islami.

Azimio hilo la Baraza la Seneti la Pakistan limesisitiza udharura wa kutatuliwa kadhia ya Palestina kwa uadilifu na insafu na kwa kutegemea maazimio ya Baraza Kuu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayotoa wito wa kuasisiwa dola huru la Palestina lenye mamlaka kamili, kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na Israel na kusitishwa ukatikli na mashambulizi dhidi ya raia wa Palestina.

Azimio hilo pia limeitaka serikali ya Pakistan kuitisha kikao maalumu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ili kusikiliza mataka ya Wapalestina na wadau wengine na kuchunguza njia za utatuzi wa kadhia hiyo.

Baraza la Seneti la Pakistan limesisitiza kuwa utatuzi wa amani wa kadhia ya Palestina utakuwa na maslahi kwa usalama na amani ya kimataiifa na kwamba kuna udharura kwa jamii ya kimataifa kuendelea kutoa misaada ya kiufundi kwa taifa la Palestina.  

Vyama na makundi yote ya Palestina yamepinga na kukataa mpango huo.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Jumanne ya tarehe 28 Januari, Rais wa Marekani, Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizindua mpango wa Muamala wa Karne katika Ikulu ya White House.

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza. 

............
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni