?>

Serikali ya Mansour Hadi: Wananchi wamejiunga na Ansarullah Yemen

Serikali ya Mansour Hadi: Wananchi wamejiunga na Ansarullah Yemen

Waziri wa Habari, utamaduni na utalii wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen amekiri kwamba wananchi wa mkoa wa Ma'rib wamejiunga na jeshi na kamati za kujitolea za wananchi na kuwataka wakazi wa mkoa huo wasiache vijana wao kujiunga na kamati hizo za kujitolea ambazo ni maarufu kwa jina la Ansarullah.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Moammar al Eryani alisema hayo jana (Jumamosi) katika mahojiano aliyofanyiwa na sherika la habari la Sabanet na huku akikiri kuwa wananchi wa mkoa wa Ma'rib wamejiunga na harakati ya Ansarullah amesema, baada ya jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen kukaribia kuukomboa mkoa huo, idadi kubwa ya wakazi wa Ma'rib wamejiunga na harakati ya Ansarullah.

Waziri huyo wa habari wa serikali iliyojiuzulu ya Mansour Hadi amewataka wazee, wakuu wa makabila na wazazi katika kila eneo hilo waache kujiunga na  Ansarullah. Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo mamluki wa Saudi Arabia wamekiri kushirikiana na genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika uvamizi wa muungano wa Saudia nchini Yemen.

Taarifa zinasema kuwa, wanamapambano wa Ansarullah wamepata ushindi na kusonga mbele katika pembe mbalimbali za mkoa wa Ma'rib katika operesheni za kuukomboa kikamilifu kutoka katika makucha ya magaidi na mamluki wa madola vamizi.

Wananchi wengi wa Yemen wanaiunga mkono Ansarullah kutokana na kuwa ni harakati ya wananchi wa nchi hiyo yenye lengo la kulirejeshea hadhi na ukombozi taifa hilo la Kiarabu.

Baadhi ya wakuu wa kusini mwa Yemen nao wametaka vijana wa maeneo hayo wasitumwe tena kwenda kuwa mamluki wa Saudi Arabia katika medani za kivita za kaskakzini, katika mpaka wa Yemen na Saudia wakisisitiza kuwa, huko ni kucheza na roho na damu za vijana wa Yemen.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni