?>

Sheikh Zakzaky akabiliwa na tuhuma mpya siku chache baada ya kuachiliwa huru

Sheikh Zakzaky akabiliwa na tuhuma mpya siku chache baada ya kuachiliwa huru

Mahakama Kuu ya Nigeria imetoa tuhuma mpya dhidi Sheikhh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ikiwa ni siku chache tu baada ya mahakama ya Kaduna kutoa hukumu ya kuachiliwa huru kiongozi huyo wa Kiislamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wakili mmoja wa mahakama ametangaza kuwa, Nigeria imetoa tuhuma mpya dhidi ya Sheikh Zakzaky kwa kumhusisha na ugaidi.

Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky bado haijazungumzia chochote kuhusiana na tuhuma hizi mpya zilizotolewa dhidi ya kiongozi wake huyo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat waliachiwa huru Jumatano iliyopita baada ya kushikiliwa mahabusu kwa kipindi cha miaka 6 na kukabiliwa na mateso na sulubu nyingi. 

Kwa mujibu wa duru za habari, baada ya vyombo vya dola kumshikilia kiongozi huyo wa kidini kwa muda wote huo, hatimaye mahakama ya nchi hiyo imemtoa hatiani Sheikh Zakzaky na mkewe kuhusiana na mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake walikamatwa Desemba 13, 2015 katika hujuma na shambulio lililofanywa na askari wa jeshi la serikali dhidi ya Husainiya iliyoko katika mji wa Zaria.

Siku hiyo aliyokamatwa Sheikh Zakzaky, vikosi vya jeshi la Nigeria viliwafyatulia risasi Waislamu waliokuwa wamekusanyika kwenye Husaniya hiyo na nyumba yake na kuwaua shahidi mamia kadhaa miongoni mwao, wakiwemo wana watatu wa kiume wa kiongozi huyo wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*