?>

Shughuli za siri za nyuklia za Wazayuni katika kivuli cha kimya na undumakuwili wa Magharibi

Shughuli za siri za nyuklia za Wazayuni katika kivuli cha kimya na undumakuwili wa Magharibi

Tarehe 8 Mei 2019, mwaka mmoja baada Marekani kujitoa bila ya sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na baada ya kuthibiti kutokuwa na faida njia zilizopendekezwa na Ulaya za kudhamini maslahi ya Iran ndani ya mapatano hayo, Jamhuri ya Kiislamu iliamua kupunguza kwa awamu 5, sehemu ya ahadi zake ndani ya JCPOA kama vinavyosema vifungu vya 26 na 36 vya makubaliano hayo ya kimataifa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sasa hivi Iran imesema kuwa, ifikapo tarehe 23 mwezi huu wa Februari yaani kesho Jumanne, itaacha kutekeleza hatua za kujitolea ndani ya JCPOA kwa mujibu wa sheria ikiwa ni uamuzi wa kiistratijia wa kuhakikisha vikwazo vinaondolewa na inalinda haki zake.

Hata hivyo, Marekani na nchi tatu za Ulaya ambazo zimeshindwa kutekeleza majukumu na ahadi zao ndani ya JCPOA zimeanza kupiga makelele mengi kuhusu mradi wa amani wa nyuklia wa Iran ili kujaribu kuficha kushindwa kwao kuheshimu ahadi zao na kujaribu kuikwamisha Iran isipiganie haki zake inavyotakiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu makelele hayo ya nchi za Magharibi kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akisema, misimamo ya nchi za Magharibi ni ya kindumilakuwili. Vile vile amelaumu kimya cha Marekani na nchi za Ulaya kuhusu kiwanda cha silaha za nyuklia cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha Dimona ambacho ndicho kiwanda pekee cha silaha za atomiki katika eneo hili.

Katika ujumbe wake huo wa Twitter, Dk Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika: "Rais wa Marekani, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Boris Johnson, Emmanuel Macron, Angela Merkel, kweli mna wasiwasi mkubwa? Mna wasiwasi? Angalau kidogo? Hivi kimsingi kuna umuhimu wowote kwenu nyinyi kusema mna wasiwasi? Mimi nilidhania ni hivyo."

Kwa upande wake, televisheni ya al Mayadeen siku ya Ijumaa ilirusha hewani picha za satalaiti zilizochukuliwa tarehe 4 mwezi uliopita wa Januari na kutangaza kuwa, kundi la kimataifa linaloshughulika na masuala hayo limethibitisha kwamba picha hizo za satalaiti zinaonesha kuweko hatua mpya za ujenzi katika kiwanda kisicho cha kisheria cha nyuklia cha Dimona katika jangwa la Naqab (Negev) kwenye ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. 

Gazeti la Uingereza la The Guardian nalo limemnukuu Paul Ludwing, mtaalamu wa masuala ya sayansi na usalama wa dunia wa Chuo Kikuu cha Princeton akisema: Inaonekana shughuli za ujenzi katika kituo cha Dimona zilianza mwezi Aprili 2019 au mwishoni mwa mwaka 2018, hivyo shughuli hizo zilianza takriban miaka miwili iliyopita.

Shirikisho la wataalamu wa Marekani nalo limethibitisha kwamba Israel ina takriban vichwa 90 vya nyuklia vilivyotengenezwa kwa Plutonium katika kinu cha maji mazito cha Dimona.

Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza kazi ya kujenga kinu cha nyuklia cha Dimona katika muongo wa 1950 kwa msaada mkubwa wa Ufaransa na kiwanda hicho kimeendelezwa kwa msaada wa Marekani.

Shughuli hizo haramu zinaendelea katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel hauruhusu wataalamu wa kimataifa wa nyuklia kukagua shughuli zake hizo na unafanya ukaidi wa kukataa hadi leo kutia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Amma madai ya uongo ya nchi za Ulaya na Marekani kuhusu shughuli za amani za nyuklia za Iran yanatolewa katika hali ambayo wakaguzi wa kimataifa wa nyuklia wanafuatilia kwa karibu mno shughuli hizo za Iran. Si hayo tu, lakini pia Tehran imekuwa ikitoa ushirikiano mzuri sana kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kiasi kwamba hata kujitolea kwake katika kutekeleza protokali ziada zinazotolewa na wakala huo umepindukia kiwango chake cha kawaida. Yote haya ni kwa ajili ya kuthibitisha kwamba, Iran haina kitu cha kuficha katika mradi wake wa amani wa nyuklia na ndio maana shughuli zake zimekuwa na kiwango cha juu mno cha usimamiaji wa kimataifa kuliko shughuli zozote nyingine za nyuklia duniani.

Kabla ya hapo pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika kuhusu majaribio ya kombara la nyuklia la Israel yaliyofanywa mwezi Disemba 2019 kwamba: "Nchi tatu za Ulaya (Ujerumani, Uingereza na Ufaransa) pamoja na Marekani, kamwe huzioni zikifungulia mashtaka kiwanda pekee cha nyuklia katika eneo la Asia Magharibi na ambacho kimsingi kimejengwa kwa muundo kamili wa kutengeneza vichwa vya nyuklia. Lakini zinakuwa wakali zinapoona Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajitengenezea silaha za kujihami ambazo zinakubalika kabisa ulimwenguni, na hakuna yeyote anayeweza kusema si silaha za kawaida."

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni