?>

Siku ambayo Jenerali Soleimani alitangaza kuangamizwa ISIS

Siku ambayo Jenerali Soleimani alitangaza kuangamizwa ISIS

Miaka minne iliyopita, tarehe 21 Novemba 2017, Meja Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, alimtumia ujumbe Ayatullah Sayyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akitangaza kuangamizwa satwa khabithi ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kundi hilo liliangamizwa baada ya kampeni ya miaka kadhaa ya kueneza ukatili, mauaji na umwagaji damu dhidi ya raia wa Syria na Iraq.

Kundi la Daesh ambalo pia hujulikana kama ISIS au ISIL liliundwa na Abu Musab al Zarqawi na lilipata umaarufu kimataifa mwaka 2014 baada ya kusukuma askari wa Iraq kutoka miji muhimu nchini humo baada ya kuuteka mji wa Mosul.

Kwa miaka kadhaa, kundi hilo lilitekeleza mauaji ya kikatili dhidi ya raia wa Iraq na Syria. Kati ya mauaji mabaya zaidi yaliyotekelezwa na ISIS ni yale ya Sinjar ambapo maelfu ya raia wa kaumi ya Izadi waliuawa kinyama. Aidha mauaji mengine yaliyotekelezwa na ISIS ni dhidi ya maafisa 2000 wa chuo cha kijeshi cha Tikrit, Iraq. Nchi za eneo zilibaini kuwa kundi la ISIS ni tishio kubwa kwa usalama wao. Hapo ndipo wakuu wa Iran walimpa jukumu Jenerali Soleimani kutoa ushauri wa kijeshi kwa majeshi ya Iraq na Syria kuhusu mbinu za kuangamiza kundi la ISIS na kulitimua kutoka ardhi ambazo zilikuwa zinakaliwa kwa mabavu na kundi hilo.

Hatimaye baada ya mapambano ya miaka kadhaa, na kufuatia kukombolewa mji wa Abu Kamal wa Syria ulio karibu na mpaka wa Iraq, bendera ya ISIS ilishuswa na bendera ya Syria ikapeperushwa. Hapo ndipo Jenerali Soleimani alitangaza kuangamizwa utawala katili wa ISIS.  Katika barua kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kamanda huyo alisema: "Mimi kama mtumishi na askari mwenye kutekeleza wadhifa kwa niaba yako katika medani hii, ninatangaza hapa kuwa, kufuatia kukombolewa mji wa Al Bukamal, ngome ya mwisho ya ISIS na bendera ya kundi hili la Kimarekani-Kizayuni imeshushwa na mahala pake kupeperushwa bendera ya Syria na kwa msingi huo satwa khabaithi na iliyolaaniwa ya ISIS imefika ukingoni."

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq. Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Mauaji hayo yalithibitisha ukweli kuwa, Marekani ni muungaji mkono mkuu wa magaidi wa ISIS.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*