?>

Silaha zawa adimu kupatikana Marekani kutokana na kukithiri mno idadi ya wanunuzi

Silaha zawa adimu kupatikana Marekani kutokana na kukithiri mno idadi ya wanunuzi

Marekani inakabiliwa na uhaba wa silaha kufuatia kuongezeka kwa kiwango kikubwa mno ununuzi wa silaha katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa, kutokana na kuongezeka mno mahitaji ya raia wanaotaka kumiliki silaha katika miji mbalimbali ya Marekani, sambamba na usambaaji wa virusi vya corona nchini humo, silaha zimekuwa adimu na kusababisha matatizo pia kwa askari polisi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kufuatia usambaaji mkubwa wa virusi vya corona, machafuko ya kijamii na kuongezeka mno vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha nchini Marekani, raia wa nchi hiyo wamelazimika kununua kwa wingi silaha na zana za kujihami.

Kanali ya televisheni ya ABC News na taasisi ya utafiti ya Hifadhi za Ukatili wa Utumiaji Silaha zimeripoti kuwa, matukio yasiyopungua 915 ya ufyatuaji risasi yalitokea katika wiki iliyoishia Julai 26 katika maeneo mbalimbali ya Marekani na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 430.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*