?>

Spika wa Bunge la Iran: Marekani imetengwa ulimwenguni

Spika wa Bunge la Iran: Marekani imetengwa ulimwenguni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria siasa za kibeberu za Marekani na kusema kuwa, Washington imekuwa ikitumia ubabe usio wa kimantiki hususan katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump, sera ambazo zimelifanya dola hilo litengwe ulimwenguni.

(ABNA24.com) Dakta Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu ya Iran (Bunge) alisema hayo Jumatatu ya jana mbele ya waandishi wa habari mjini Beirut Lebanon na kusisitiza kwamba, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimekuwa sababu na ustawi na maendeleo ya taifa hili la Kiislamu katika nyanja mbalimbali.

Spika Larijani ameeleza kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatuma nje ya nchi bidhaa zisizo za nishati ya petrol zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 40.

Dakta Larijani ameashiria pia uwezo wa Iran na Lebanon kwa ajili ya kupanua ushirikiano wao katika uga wa kiuchumi na kueleza bayana kwamba, Tehran iko tayari kuipatia tajiriba na uozefu wake Beirut katika nyanja za kilimo na petrokemikali na kushiriki katika miradi ya pamoja.

Dakta Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia pia mpango wa Marekani-Kizayuni wa Muamala wa Karne na kusema kuwa, mpango huo umezaliwa hali ya kuwa umekufa hivyo hautakuwa na matunda yoyote.

Kadhalika Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za Kiarabu za eneo na kwamba, baadhi ya nchi za Asia Magharibi zimehadaika na hila na hadaa za Marekani, kwani licha ya kuwa huzungumzia nyuma ya pazia suala la kutaka kufanya mazungumzo yenye lengo la kuweka kando hitilafu, lakini mbele ya vyombo vya habari zinatoa matamshi ya kushangaza.

..........
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni