?>

Taarifa ya IRIB Kimataifa kufuatia kuuawa shahidi mwandishi habari Mpalestina

Taarifa ya IRIB Kimataifa kufuatia kuuawa shahidi mwandishi habari Mpalestina

Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kimelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumuua shahidi mwandishi habari Mpalestina

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirin Nasri Abu Aqleh mwandishi habari Mpalestina wa Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel alipokuwa akiakisi machafuko katika kambi ya wakimbizi Wapalestina mjini Jenin.

Katika taarifa yake  Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeelezea masikitiko yake sambamba na mshikamano wake na waandishi wa habari huru wa dunia ambao wanatoa taarifa za ukweli na za wazi kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni  na wala hawapuuzi hatua zisizokubalika za utawala huo ghasibu.

Taarifa hiyo imelaani vikali  hatua ya jeshi la Kizayuni ya kuwaua waandishi wa habari ili wasiakisi yale wanayofanyiwa wananchi madhulumu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hasa  Quds Tukufu (Jerusalem).

Halikadhalika taarifa hiyo imeongeza kuwa, utawala utendao jinai wa Israel si tu kuwa umetanda jinai kama hiyo dhidi ya waandishi habari, bali pia hata madaktari, wauguzi na wengine wengi ambao wamekuwa wakilengwa na vikosi vya utawala wa Kizayuni.

Aidha Kitengo cha Kimataifa cha IRIB kimesema kuuawa Shirin Nasri Abu Aqleh mjini Jenin wakati akitekeleza kazi yake ya upashaji habari, kutabakia hai katika kumbukumbu sawa na walivyobakia hai katika kumbukumbu mashahidi na wahanga wengine wa jinai za utawala wa Kizayui dhidi ya haki za binadamu, ubinadamu na uhuru.

Taarifa hiyo ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema:"Waandishi habari wa kanali za Kitengo cha Kimtaifa cha IRIB pia  kwa mara kadhaa wamekuwa katika medani hatari  kufichua mienendo ya utawala bandia wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na nchi za eneo , ambapo wamepata madhara katika kazi yao."  Kwa msingi huo waandishi habari wa Kitengo cha Kimataifa cha IRIB nao pia wanatangaza kufungamana na  familia na kundi kubwa la waandishi wa habari waliouawa shahidi , kudhulumiwa na kudhuriwa na utawala wa Kizayuni. Kumbukumbu ya waandishi habari mashahidi na wanaharakati wote daima itabakia hai katika nyoyo za wafanyakazi wa kanali za Press TV, Al-Alam, Hispan TV, n.k.

Vikosi vya Israel vimewakamata, kuwajeruhi au kuwauwa shahidi mamia ya waandishi wa habari hadi sasa. Hivi karibuni Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari wa Palestina ilieleza kuwa, hatua za kiuadui za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wa habari zinalenga kuficha jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*