?>

Tamasha la wanawake wanaodansi "Samba" barabarani Jazan lazusha taharuki Saudia

Tamasha la wanawake wanaodansi

Kuonyeshwa taswira za wanawake wanaodansi katika bararaba za mji wa Jazan nchini Saudi Arabia kumezusha taharuki na makelele mengi ya upinzani katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pamoja na hasira na manung'uniko ya wananchi dhidi ya utendaji wa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vyombo mbalimbali vya habari vimeakisi wimbi la hasira za wananchi wa Saudia dhidi ya burudani zilizoanzishwa na Mohammad bin Salman, mrithi wa ufalme anayehisabika pia kama kiongozi halisi wa nchi hiyo, baada ya kuonekana wanawake wanaocheza dansi maarufu ya Brazil ya Samba wakiwa nusu utupu katika barabara za mji wa bandari wa Jazan kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa duru za habari, onyesho hilo la Samba ni sehemu ya tamasha la msimu wa baridi  la Jazan lililoandaliwa na viongozi wa utawala wa Aal Saud kama sehemu ya programu ya starehe na burudani zinazofanyika katika kila pembe ya Saudi Arabia.

Programu za starehe na burudani ni sehemu kuu ya malengo ya mwaka 2030 yaliyoandaliwa na utawala wa kihafidhina wa Saudia chini ya uongozi wa Mohammad bin Salman kwa ajili ya kuifanya nchi hiyo iondokane na utegemezi wa mafuta na kuboresha haiba yake kimataifa.

Katika kulalamikia hatua hiyo ya viongozi wa utawala wa Aal Saud ya kuanzisha programu ya starehe na burudani zinazokinzana na maadili ya kidini, mwanaharakati mmoja ameandika katika mitandao ya kijamii: "Saudi Arabia, ambayo ni mahali yalipo maeneo matakatifu zaidi ya Kiislamu, imekengeuka misingi ya Kiislamu".../ 342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*