?>

Tanzania: Msichonganishe Serikali mapambano dhidi ya corona

Tanzania: Msichonganishe Serikali mapambano dhidi ya corona

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Doroth Gwajima amesema kuwa, uchonganishaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa Serikali ya awamu ya tano na sita katika mapambano dhidi ya Covid-19, hauna maana.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waziri Gwajima ameeleza kuwa, mapambano  ya Covid-19 Serikali zote zina lengo moja nalo ni kutokomeza ugonjwa huo .

Tabia mbaya inayoanza kujitokeza nchini ni mtu kuchonganisha Serikali katika mapambano dhidi ya corona,” amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Amesema katika vita dhidi ya Covid- 19, Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza mapambano pale ilipoishia Serikali iliyopita kwa kujiridhisha kwanza katika masuala ya chanjo kwa kuunda kamati ya wataalamu ili kujiridhisha.

“Serikali (iliyopita) ilisema tusikimbilie chanjo tujiridhishe na Rais Samia  amekuja na mkakati wa kujiridhisha, mpango ambao umesifiwa na watu wa mataifa mbalimbali. 
 “Baada ya kamati iliyoundwa kutoa taarifa yake na kujiridhisha pia kuangalia mataifa mengine ambayo tayari yamekwishapata chanjo tumesaini mikataba ya kuwekwa kwenye orodha.”

Kuhusu suala la “ Lockdown” Waziri Gwajima alisema Tanzania haina mpango wa kuweka wananchi wake “Lockdown” na kusisitiza kuwa watawekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amewasisitiza wananchi kuendelea kuchua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kama inavyoshauriwa na wataalamu ikiwamo kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na  kujiepusha na misongamano isiyo ya lazima.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*