?>

Trump aliacha kwa makusudi maambukizo ya corona yaongezeke Marekani baada ya kubwagwa katika uchaguzi

Trump aliacha kwa makusudi maambukizo ya corona yaongezeke Marekani baada ya kubwagwa katika uchaguzi

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa la Magonjwa ya Kuambukiza ya nchini Marekani amesema kuwa, rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump aliacha kwa makusudi maambukizo ya ugonjwa wa COVID-19 yaongezeke nchini humo baada ya kubwagwa katika uchaguzi wa Novemba 3, 2020.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Gazeti la Independent limemnukuu Anthony Fauci akisema hayo Ijumaa katika mahojiano maalumu na gazeti hilo na kuongeza kuwa, baada ya kushindwa na Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa Novemba 2020, Donald Trump aliacha kabisa kukabiliana na kirusi cha corona katika wiki kadhaa za mwishoni mwa serikali yake.

Lilipoanza wimbi la maambukizi ya corona, Trump alizembea kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na wimbi hilo. Alidharau na kukejeli maonyo yaliyotolewa na wataalamu wa afya na aliendelea kushiriki katika mikutano ya hadhara kama kawaida huku akiita COVID-19 kwa dharau kuwa ni kirusi cha China.

Matokeo yake ni kuwa hivi sasa Marekani ndiyo inayoongoza dunia kwa mbali kwa idadi kubwa kupindukia ya wagonjwa na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ambao ni janga la dunia nzima. Hadi jana usiku, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 walioripotiwa rasmi na serikali ya Marekani walikuwa wameshapindukia 28,606,256 huku idadi ya Wamarekani waliokufa kwa ugonjwa huo hadi jana usiku ikiwa ni zaidi ya 507,795. Siasa hizo mbovu ni miongoni mwa sababu kuu za kubwagwa vibaya Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani uliofanyika tarehe 3 Novemba, 2020.

Hadi hivi sasa idadi ya vifo na maambukizo ya corona ni kubwa nchini Marekani, na sehemu kubwa ya lawama za hali hiyo anabebeshwa Donald Trump ambaye alifikia hata kuacha Wamarekani wazidi kuambukizwa corona baada ya kushindwa katika uchaguzi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni