?>

Trump: Biden anaielekeza kadhia ya Ukraine kwenye Vita Vikuu vya Dunia

Trump: Biden anaielekeza kadhia ya Ukraine kwenye Vita Vikuu vya Dunia

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump amemtuhumu rais wa nchi hiyo Joe Biden kuwa hana uwezo katika uendeshaji uchumi wa nchi na kusema kuwa katika kadhia ya Ukraine, kiongozi huyo anaielekeza Marekani kwenye Vita Vikuu vya Dunia.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Trump ameyasema hayo katika mahojiano na tovuti ya habari ya Newsmax, ambapo mbali na kukosoa sera ya serikali ya Biden ya kupeleka silaha Ukraine ameongeza kuwa, sera za aina hiyo zinashadidisha mapigano katika eneo na kusababisha vita vikuu vingine vya dunia.

Trump amesema: "kama mimi ningekuweko madarakani vita vya Ukraine visingetokea katu".

Hata hivyo rais huyo wa zamani wa Marekani hakubainisha ni vipi angeliweza kuzuia vita kati ya Russia na Ukraine visitokee.

Trump ameeleza pia kwamba serikali iliyoko madarakani nchini Marekani ndiyo iliyosababisha ughali wa bidhaa ambao haujawahi kushuhudiwa nchini humo na kupanda kwa bei ya mafuta pia na akadai kwamba, kuongezeka gharama za mafuta kumetokana na sera mbovu ya Biden katika uzalishaji wa nishati za kijani ndani ya nchi hiyo.

Sambamba na kuthibitisha na kutoa hakikisho kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2024, rais huyo wa zamani wa Marekani amesema: "nchi yetu ina mtatizo mengi na haijawahi hapo kabla kukabiliwa na matatizo kama haya".../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*