?>

Trump kuburuzwa tena bungeni; Pelosi: Trump lazima atimuliwe madarakani

Trump kuburuzwa tena bungeni; Pelosi: Trump lazima atimuliwe madarakani

Baraza la Wawakilishi la Marekani, jana lilipasisha muswada wa kuburuzwa tena bungeni rais wa nchi hiyo, Donald Trump ili akasailiwe.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, muswada huo umepasishwa kwa kura 229 za ndio na 197 za hapana.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, wabunge 10 wa chama cha Republican, cha Donald Trump, nao wameunga mkono mpango wa kuburuzwa bungeni Trump kwa ajili ya kusailiwa.

Kwa kupasishwa muswada huo, Trump amekuwa rais wa kwanza kabisa katika historia ya Marekani kuitwa mara mbili bungeni kwa ajili ya kusailiwa akiwa bado madarakani.

Muswada huo wa kuburuzwa bungeni Trump sasa utapelekwa mbele ya Baraza la Sanate kwa ajili ya kupasishwa na baadaye kuanza kuhukumiwa Trump.

Nany Pelosi, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema kwenye kikao cha kupasishwa muswada wa kumburuza bungeni Trump kwamba, rais huyo wa Marekani lazima atimuliwe madarakani. Spika huyo wa bunge amesema, Trump ni hatari ya wazi kabisa kwa Marekani.

Kikao cha kupasisha muswada huo kilichelewa kuanza kutokana na uchochezi wa wafuasi wa Trump waliotishia kulivamia jengo la Congress.

Itakumbukwa kuwa, Jumatano, Januari 6, 2020 wakati mabaraza mawili ya Congress, lile la wawakilishi la lile la sanate yalipokuwa kwenye kikao cha pamoja cha kupasisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, magenge ya wafuasi wa Donald Trump yalivamia jengo hilo na kufanya mauaji na uharibifu. Uvamizi huo ulitokea baada ya Trump kuwachochea wafuasi wake wakusanyike mbele ya jengo la Congress. Watu watano waliuawa kwenye uvamizi huo.

Hillary Clinton, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani ambaye pia alikuwa mgombea urais wa uchaguzi wa kabla ya uliopita amesema kuwa, magenge ya Trump yaliyovamia jengo la Congress na kufanya mauaji ni ya kigaidi. 

Licha ya fujo zote hizo za wafuasi wa Donald Trump, lakini Baraza la Congress la Marekani lilipasisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa Rais wa Novemba 3, 2020.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*