?>

Trump kufungwa miaka 10 jela iwapo atapatikana na hatia ya kuchochea shambulizi dhidi ya Kongresi

Trump kufungwa miaka 10 jela iwapo atapatikana na hatia ya kuchochea shambulizi dhidi ya Kongresi

Ripoti zinasema kuwa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, yumkini akahukumiwa kifungo cha miaka kumi jela iwapo atapatikana na hatia ya kuhusika na shambulizi lililofanywa na wafuasi wake dhidi ya majengo ya Kongresi ya nchi hiyo licha ya Baraza la Seneti la Marekani kukwamisha muswada wa kumtia hatiani kwa tuhuma za kuchochea shambulizi hilo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hii ni baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Trump yumkini akafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kuhusika na shambulizi la tarehe 6 mwezi uliopita wa Januari dhidi ya majengo ya Kongresi ya nchi hiyo. 

Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeandika kuwa, juhudi za wapinzani wa Donald Trump dhidi ya mwanasiasa huyo hazijasita na kuongeza kuwa, Trump bado anakabiliwa na hatari ya kuswekwa jela licha ya kuondolewa hatiani katika kikao cha kumsaili kwenyeBaraza la Seneti.

Limeandika kuwa sababu ya kutotiwa hatia Trump katika kikao cha pili cha Baraza la Seneti ni uaminifu wa wanachama wa chama cha Republican kwa Donad Trump na kuongeza kuwa: Japokuwa idadi kubwa ya Warepublican akiwemo kiongozi wa chama hicho katika Seneti ya Marekani, Mitch McConnell walipiga kura ya kumuondoa hatiani Trump lakini McConnell mwenyewe anasisitiza kuwa, madhui ya kikao hicho cha kusailiwa Trump haikuwa suala la kumuondoa hatiani. 

Ripozi zinasema inaonekana kuwa, Mitch McConnell ambaye hapo kabla alimkosoa vikali Donald Trump, sasa ameridhishwa na ushahidi wa kuhusika kwake na uchochezi wa machafuko na uasi nchini Marekani. 

Iwapo atapandishwa kizimbani, Donald Trump yumkini akahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni