?>

Tunisia: Hakuna mashinikizo ya kututaka tuanzishe uhusiano wa kawaida na Israel

Tunisia: Hakuna mashinikizo ya kututaka tuanzishe uhusiano wa kawaida na Israel

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Tunisia amesema kuwa, hakuna mashinikizo yoyote kutoka upande wowote ule ili nchi hiyo ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Othman Jerandi, amesaema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni mjini Tunis ambapo amesisitiza kuwa, nchi hiyo haijaandamwa na mashinikizo yoyote ili ianzishe uhusiano wa kawaida na Israel.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Tunisia amesema kuwa, nchi yake haijatakiwa na upande wowote ule ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba, kila nchi iko huru kuchukua maamuzi itakayo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Tunisia iliashiria juhudi za baadhi ya mataifa ya kieneo za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, serikali ya Tunis haina mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.

Hivi karibuni, Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel tokea mwezi Agosti wakati mtawala wa Marekani anayeondoka, Donald Trump alipoanzisha mkakati wa kuzishinikiza nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala huo bandia.

Mbali na Morocco, nchi zingine za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na Israel hivi karibuni ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala huo dhalimu katika fremu ya njama za Marekani-Kizayuni za kudhoofisha uungaji mkono wa nchi za Kiarabu kwa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*