?>

Tutu: Biden aache kuficha na kufadhili silaha za nyuklia za Israel

Tutu: Biden aache kuficha na kufadhili silaha za nyuklia za Israel

Katibu Mkuu wa zamani wa Baraza la Makanisa ya Afrika Kusini Askofu Desmond Tutu amemtaka rais mteule wa Marekani Joe Biden kuacha kukingia kifua silaha za nyuklia za Israel na kusitisha ufadhili mkubwa wa Washington kwa miradi ya silaha za nyuklia ya utawala huo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Desmond Tutu ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel amesema katika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Guardian la Uingereza kwamba, kuna ulazima wa kukomeshwa usiri kuhusu silaha za nyuklia za Israel na ufadhili wa fedha nyingi kwa utawala unaotekeleza siasa za kuwakandamiza Wapalestina; mchezo huu unapaswa kukomeshwa, na serikali ya Marekani inalazimika kushikamana na sheria zake na kukata misaada yake kwa Israel. 

Tutu ambaye aliongoza tume ya kutafuta ukweli na suluhu nchini Afrika Kusini ameongeza kuwa: Serikali ijayo ya Biden inapaswa kutekeleza sheria za Marekani kwa njia sahihi na kuitambua Israel kama nchi inayoeneza silaha za nyuklia eneo la Mashariki ya Kati. 

Desmond Tutu amesema kuna uwezekano kwamba miongoni mwa sababu za kubakia nakala ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa Israel zaidi ya kipindi cha utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini  ni kwamba Israel imeweza kuendeleza mfumo wake wa ukandamizaji si kwa kutumia bunduki za wanajeshi pekee, bali pia kwa kuendelea kuelekeza silaha zake za nyuklia kwenye vichwa vya mamilioni ya wanadamu. 

Vilevile Tutu ameikumbusha Marekani Sheria ya Leahy (Leahy Law) inayoizuia serikali ya Washington kutoa misaada ya silaha kwa tawala zinazokiuka haki za binadamu kwa mpangilio maalumu. Amekumbusha kwamba serikali ya Jimmy Carter ilikataa kutoa misaada kwa India na Pakistan kwa hoja kwamba sheria inazuia kutoa misaada ya kiuchumi na kijeshi kwa nchi zinazosambaza na kumiliki silaha za nyuklia. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*