?>

Ubalozi wa Palestina Tehran walaani uhasama wa Uingereza dhidi ya Hamas

Ubalozi wa Palestina Tehran walaani uhasama wa Uingereza dhidi ya Hamas

Ubalozi wa Palestina mjini Tehran umetoa taarifa na kulaani vikali hatua ya Uingereza ya kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika orodha ya makundi ya 'kigaidi'.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa hiyo imesema badala ya uhasama huo serikali ya Uingereza inapaswa kutambua rasmi uhuru wa Palestina.

Aidha Ubalozi wa Palestina mjini Tehran umesema nchi ambazo zinatambua taifa la Palestina ni zaidi ya nchi ambazo zimeutambua utawala wa Kizayuni wa Israel. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Uingereza ndio chanzo cha matatizo ya taifa la Palestina kwa muda wa miaka 73 sasa. 

Ikumbukwe kuwa, katika kuendeleza siasa zake dhidi ya taifa la Palestina na kuunga mkono utawala haramu wa Israel, Uingereza imetuhumu na kuitangaza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Paletina Hamas kuwa ni kundi la kigaidi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*