?>

Uchaguzi wa mapema; chaguo la Ennahdha iwapo muafaka wa kisiasa hautafikiwa huko Tunisia

Uchaguzi wa mapema; chaguo la Ennahdha iwapo muafaka wa kisiasa hautafikiwa huko Tunisia

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Tunisia na ambaye pia ni mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama cha Ennahdha amesema kuwa chama hicho kinaunga mkono chaguo la kufanyika uchaguzi wa mapema wa Rais na Bunge iwapo hakutafikiwa mapatano.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rafik Abdul Salam ameasahiria matukio ya karibuni nchini Tunisia baada ya Rais Kais Saeid wa nchi hiyo kuchukua uamuzi wa kumfuta kazi Waziri Mkuu na kusitisha shughuli za Bunge na kueleza kuwa: Hakuna njia nyingine isipokuwa kuitisha uchaguzi wa mapema wa Rais na Bunge iwapo muafaka wa kisiasa hautapatikana. 

Rais Kais Saeid wa Tunisia tarehe 25 mwezi Julai mwaka huu alimfuta kazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hicham Mechichi na kisha kulivunja Bunge na akasema amechukua hatua hiyo katika juhudi za kurejesha amani na uthabiti nchini Tunisia.

Rais Saeid wa Tunisia amehalalisha hatua hiyo na kusema kwamba, amechukua maamuzi hayo ili kurejesha utulivu wa kijamii na kuinusuru nchi. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*