?>

Uchaguzi wa Rais na Bunge unafanyika leo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Uchaguzi wa Rais na Bunge unafanyika leo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanashiriki katika uchaguzi mkuu kwa ajili ya kumchagua Rais na wawakilishi wa Bunge.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi ya leo huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea machafuko.

Rais Faustin-Archange Touadera anachuana na wagombea wengine zaidi ya kumi kuwania kiti cha urais. Mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo ni Anicet Georges Dologuele aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa, uchaguzi wa Rais utaingia duru ya pili, endapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50.

Hivi karibuni Russia na Rwanda zilituma nchini humo mamia ya wanajeshi baada ya kuibuka madai ya kuweko njama za mapinduzi ya kijeshi kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais na Bunge wiki ijayo.

Hivi karibuni wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSCA wakishirikiana na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, walifanikiwa kuwafurusha waasi katika mji wa Bambari uliokuwa umetekwa na waasi hao.

Machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yalizuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, François Bozizé. Baada ya Rais Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi wa Kikristo wenye misimamo ya kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu ya Waislamu waliuawa na wengine wengi kulazimika kuwa wakimbizi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni