?>

Uchaguzi wa rais nchini Iran wamalizika baada ya upigaji kura wa masaa 19

Uchaguzi wa rais nchini Iran wamalizika baada ya upigaji kura wa masaa 19

Uchaguzi wa urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umemalizika mapema leo asubuhi baada ya upigaji kura wa masaa 19 ambapo mamilioni ya wapiga kura wamejitokeza.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa, upigaji kura umemalizika Jumamosi (Juni 19) saa nane usiku, masaa 19 baada ya vituo vya upigaji kura kufunguliwa saa moja asubuhi Ijumaa, Juni 18.

Zoezi la upigaji kura liliongezwa muda mara kadhaa ili kuhudumia idadi kubwa ya wapiga kura na pia kutokana na uzingatiaji wa kanuni za kiafya za kuzuia kuenea corona.

Hivi sasa zoezi la kuhesabu kura linaendelea na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran inatazamiwa kuanza kutangaza matokeo hatua kwa hatua.

Zaidi ya Wairani milioni 59 walikuwa wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ambao ulikuwa wa wagombea wanne ambao ni Erahim Raisi, Mohsen Rezaei, AbdulNasser Hemmati na Amir-Hossein Ghazizadeh-Hashemi. Wagombea wengine watatu walijiondoa katika mchuano huo Jumatano.

Rais wa sasa Hassan Rouhani ambaye anamaliza muhula wake wa pili mfululizo haruhusiwi kisheria kugombea awamu hii ya urais.

Tangu dakika za mwanzoni kabisa mwa kuanza zoezi la kupiga kura jana katika kona zote za Iran na kushiriki Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika dakika za awali kabisa za zoezi hilo, vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iran vimeakisi kwa kiwango kikubwa uchaguzi huo na vingi vimeonesha picha za mubashara wakati wimbi kubwa la wananchi wa Iran lilipojitokeza katika vituo mbalimbali kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wao.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*