?>

Ugomvi baina ya Russia na Wazayuni waongezeka, Moscow yakabidhi kambi zake kwa Iran

Ugomvi baina ya Russia na Wazayuni waongezeka, Moscow yakabidhi kambi zake kwa Iran

Gazeti la Times la linalochapishwa mjini Moscow limeandika kuwa, Russia imeanza kuondoa wanajeshi wake nchini Syria na inakabidhi kambi zake kwa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya al Alam imelinukuu gazeti hilo ambalo lina ofisi zake katika miji mikuu ya Uholanzi na Russia ya Amsterdam na Moscow likiandika kuwa, kambi za jeshi la anga la Russia huko Syria sasa zitakuwa mikononi mwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na Hizbullah ya Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Russia wanaondolewa nchini Syria kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu za jeshi la Russia huko Ukraine na hadi hivi sasa kambi kadhaa za kijeshi zilizokuwa mikononi mwa jeshi la anga la Russia katika kona mbalimbali za Russia zimeshakabidhiwa kwa jeshi la Iran la SEPAH na Hizbullah ya Lebanon.

Gazeti hilo limeongeza kuwa, Russia ilikuwa na wanajeshi 63,000 huko Syria na kwamba zoezi la kuwapunguza wanajeshi hao kwa ajili ya kuongeza nguvu za wanajeshi wake nchini Ukraine limekuwa likifanyika kwa muda tena.

Jambo hilo linaonesha kuzidi kuwa mbaya uhusiano wa Russia na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na utawala huo kusaidiana na nchi za Magharibi kuifanyia uadui Russia kutokana na vita vya Ukraine.

Hatua hiyo ya Russia imewatia kiwewe viongozi wa Israel kiasi kwamba Ehud Yari, mtaalamu Mzayuni ameiambia kanali ya 12 ya televisheni ya Israel kuwa, sasa Iran itakuwa na ushawishi mkubwa zaidi nchini Syria na hilo ni hatari sana kwa utawala wa Kizayuni.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*