?>

Uhusiano wa Misri na Libya wazidi kuonesha ishara za kuboreka

Uhusiano wa Misri na Libya wazidi kuonesha ishara za kuboreka

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Libya na Misri wamefanya mazungumzo ya simu katika juhudi za kuboresha ushirikiano baina yao baada ya miaka mingi ya mgogoro katika uhushiano baina ya pande mbili.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mazungumzo ya simu baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry na waziri mwenzake wa Libya, Mohamed al Taher Siala yamefanyika baada ya jana Jumatatu kutangazwa habari kwamba, karibuni hivi serikakli ya Misri itafungua tena ubalozi wake katika nchi jirani ya Libya. Mohammed al Qablawi.

Msemaji wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya amethibitisha habari hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa Misri uliotembelea Libya na kuongeza kuwa, Cairo imeahidi kwamba karibuni tu hivi ubalozi wa Misri utafunguliwa mjini Tripoli.

Akihojiwa na mtandao wa habari wa Arabi 21, Mohammed al Qablawi amesema, lengo la ziara ya ujumbe huo wa Misri nchini Libya ni kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi mbili.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*