?>

Uingereza yalaani mahakama iliyozuia wakimbizi kupelekwa Rwanda kwa nguvu

Uingereza yalaani mahakama iliyozuia wakimbizi kupelekwa Rwanda kwa nguvu

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Priti Patel amelaani vikali uamuzi wa Mahakama ya Ulaya inayoshughulikia Haki za Binaadamu, ECHR wa kuzuia safari ya kwanza ya ndege ya Uingereza kuwapeleka nchini Rwanda waomba hifadhi.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Katika mahojiano ya Jumamosi na gazeti la The Telegraphm Patel amedai kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ni "kashfa," Ameendelea kudai kuwa mahakama hiyo ilifanya kazi kwa njia isiyo ya wazi.

 Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Dominic Raab alisema Alkhamisi kwamba Uingereza haina mpango wa kujiondoa kwenye Mahakama ya ECHR, lakini aliongeza kuwa mahakama hiyo iliyoko Strasbourg, imevuka mamlaka yake katika kuzuia uhamishaji huo.

Kuingilia kati kwa kuchelewa mahakama ya Ulaya kumesababisha baadhi ya watu kutoka chama cha Kihafidhina cha Waziri Mkuu Boris Johnson kutoa wito kwa Uingereza kujiondoa kabisa katika Mahakama ya Ulaya inayoshughulikia Haki za Binaadamu.

Mpango huo wa Uingereza wa kuwapelekea wakimbizi Rwanda kwa nguvu bila hiari yao umekosolewa vikali. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, ametupilia mbali uamuzi wa serikali ya Uingereza wa kuwahamishia Rwanda watafuta hifadhi wanaokwenda nchini humo huku akisema makubaliano hayo ya kando kati ya nchi mbili hizo ni makosa.sawa na kufunguliwa ukurasa wa giza katika haki za kimataifa za wakimbizi.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi ameendelea kubainisha kuwa, Rwanda ilikuwa na historia ya kipekee ya kukaribisha na kusaidia maelfu ya wakimbizi kutoka DRC na Burundi, na akaongezea kwa kusema, nchi hiyo haina uwezo na miundombinu ya kuhudumia wakimbizi kwa kuzingatia mahitaji ya sasa.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*