?>

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Japan

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Japan

Idadi ya Waislamu wanaoishi nchini Japan, ingawa ni ndogo, imeongezeka maradufu katika muongo moja uliopita kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 230,000 mwishoni mwa mwaka 2019.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Miongoni mwa idadi hiyo kuna Wajapani 50,000 waliosilimu nukta inayoashiria namna Uislamu unavyoendelea kuwavutia raia wengi wa nchi hiyo ya  Asia Mashariki.

Kwa mujibu wa tovuti ya goodmenproject.com, pamoja na kuwa Japan kaitka miaka ya nyuma haikuwa nchi yenye kuwakaribisha sana Waislamu, katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo imebadili muelekeo na sasa inawakumbatia Waislamu na utamaduni wao.

Katika miongo ya karibuni Japan imeshuhudia ongezeko la wahajiri rasmi kutoka nchi za Kiislamu kama vile Iran, Pakistan, Indonesia, na Bangladesh ambao walifika nchini humo kama wafanyakazi. Wengi walifanya kazi katika sekta ya ujenzi na taaluma nyinginezo. Ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya wahajiri hao, misikiti imeongezeka kote Japan.

Ongezeko la misikiti limepelekea Wajapan wengi wasiokuwa Waislamu kupata sehemu ya kuuliza maswali kuhusu Uislamu kwani wengi wamekuwa wakitegemea vyombo vya habari vyenye kupotosha. Hivyo misikiti nchini Japan ni vituo muhimu vya kutoa mafunzo kwa wasiokuwa Waislamu.  Aidha kutokana na kuwa Japan ina mkakati maalumu wa kuwavutia watalii na wafanyabiashra kutoka nchi za Kiislamu, nchi hiyo sasa ina migahawa na hoteli zenye kutoa huduma za halali kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni