?>

Ujumbe wa maneva ya kijeshi ya Iran na Russia: Kuimarishwa amani, urafiki na usalama katika eneo

Ujumbe wa maneva ya kijeshi ya Iran na Russia: Kuimarishwa amani, urafiki na usalama katika eneo

Maneva ya usalama wa baharini kati ya Iran na Russia katika mwaka huu wa 2021 ilianza jana Jumanne asubuhi katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi na Bahari ya Oman.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Je, maneva hiyo ambayo imepangwa kuendelea kwa siku mbili inakusudia kufikia malengo yapi na ina umuhimu gani?

Ni wazi kuwa kudhaminiwa usalama wa njia za meli katika bahari ya Hindi ni dhamana kubwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya kiuchumi katika upeo wa kimataifa. Umuhimu wa maneva hiyo ambayo inafanyika katika eneo lenye ukubwa wa kilomitamraba 17,000 chini ya kauli mbiu ya 'Ushirikiano wa Pamoja Baharini kwa ajili ya Usalama wa Biashara Baharini', unaweza kutathminiwa katika mtazamo huo.

Akizungumzia suala hilo, Admeli Ghulamreza Tahani, msemaji wa maneva hiyo amesema malengo yanayofuatiliwa katikama maneva hiyo ni kuimarisha usalama katika sekta ya uokoaji na ufikishaji misaada ya kibinadamu, kupeana uzoefu na kuonyesha usirikiamo wa vikosi vya majini vya Iran katika ngazi za kimataifa.

Kufanya maneva za pamoja na nchi nyingine ni moja ya stratejia za Iran kwa ajili ya kuimarisha usalama na amani katika eneo. Kwa msngi huo Iran hufanya maneva nyingi kila mwaka katika bahari za Oman na India.

Katika uwanja huo, Ali Ismail Ardekani, mchamchuzi wa masuala ya kisiasa anasema: Iran na Russia zimefikia natija hii kwamba kwa kusaidiana na kupitia ushirikiano wao wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi zinaweza kuizuia Marekani isifikie malengo yake. Hii ni pamoja na kuwa kukabiliana na matakwa ya Marekani yaliyo nje ya sheria, katika nyanja za kisiasa, kiusalama na kiuchumi kunaweza kuandaa uwanja wa kufikiwa mapatano juu ya udharura wa kulazimishwa nchi hiyo ya Magharibi kubadilisha mienendo yake kuhusu masuala mengine ya kimataifa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vikali siasa za upande mmoja katika ngazi za kimataifa. Inaamini kuwa usalama wa eneo unapaswa kudhaminiwa kwa pamoja na mataifa ya eneo hili. Ni kwa msingi huo ndipo Iran ikatoa pendekezo la nchi husika za Ghuba ya Uajemi kudhamini usalama wa eneo kupitia mpango wa 'Ubunifu wa Amani ya Hormoz.' 

Maeneo ya kistratejia katika pembe zote za dunia yana umuhimu mkubwa kwa kutilia maanani mfungamano uliopo kati ya maeneo hayo na uchumi wa dunia.

Ni katika mtazamo huo ndipo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikaimarisha uwezo wa meli na manowari zake kwa ajili ya kusaidia katika kuimarisha usalama wa meli za biashara na kupambana na magenge ya wahalifu na maharamia baharini.

Kwa msingi huo, maneva ya hivi sasa ya baharini kati ya Iran na Russia inaweza kutathminiwa katika mitazamo miwili.

Wa kwanza ni kuimarisha usalama kwa kushirikishwa nchi za eneo. Kuhusu hilo, mwezi Disemba uliopita, Iran, Russia na China zilifanya maneva ya pamoja baharini katika eneo la Bandari ya Shahid Rajai, ambayo ilikuwa na umuhimu maalum.

Mtazamo wa pili kuhusu umuhimu wa maneva ya kijeshi kati ya Iran na Russia ni kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa madhumuni ya kukabiliana na kila aina ya vitisho dhidi ya usalama wa meli za biashara baharini. Kufikia sasa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameweza kutekeleza operesheni muhimu na maneva tofauti kwa ajili ya kulinda usalama baharaini. Kupitia maneva hizo ambazo zimefanyika katika maji ya kimataifa na pia karibu na mipaka yake ya majini, Iran imeweza kupiga hatua kubwa katika kudhamini usalama wa baharini. Kwa mtazamo huo, tunaweza kusema kuwa ujumbe wa maneva ya pamoja kati ya Iran na Russia ni kuimarisha amani, urafiki na usalama katika eneo.

342/
Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni