?>

Ukatili wa majumbani waongezeka Marekani katika kipindi cha corona, matumizi ya pombe yatajwa kuwa sababu

Ukatili wa majumbani waongezeka Marekani katika kipindi cha corona, matumizi ya pombe yatajwa kuwa sababu

Gazati la Washington Post limeripoti kuwa, ukatili wa ndani ya familia umeongeza nchini Marekani katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya corona kutokana na kukithiri kwa matumizi ya vileo na pombe.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti ya Washington Post imesema kuwa, utafiti wa hivi karibuni ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya jinai na wachumi mawili umeonesha kuwa, mara zote utumiaji wa pombe na vileo unapokuwa rahisi na mwepesi, vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu pia huongezeka. 

Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa, kesi za kukamatwa watu kwa tuhuma za ukatili zimeongezeka sana baina ya watu wenye zaidi ya miaka 21 wanaoruhusiwa kutumia vileo na pombe nchini Marekani. 

Wataalamu wanasema kuwa kafyu na sheria zinazowazua watu kutoka nje katika kipindi cha maambukizi ya corona, mashikinikizo ya kinafsi ya kipindi hiki na ulevi unaofanyika majumbani bila ya usimamizi wa vyombo vya salama, vimezidisha visa vya uhalifu na katili ndani ya familia za Wamarekani. 

Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na kesi nyingi zaidi za maambukizi ya corona na vilevile idadi kubwa zaidi ya watu walioaga dunia kutokana na gonjwa wa Covid-19.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*