?>

Ukwamishaji mpya wa Marekani dhidi ya juhudi za Iran za kupambana na virusi vya corona

Ukwamishaji mpya wa Marekani dhidi ya juhudi za Iran za kupambana na virusi vya corona

Baada ya kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA hapo mnamo Mei 2018, na katika fremu ya kile kinachotajwa kuwa 'mashinikizo ya juu kabisa', Marekani imekuwa ikitekeleza vikwazo vikali zaidi katika historia yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wala haijawahi kulegeza vikwazo hivyo vya kinyama hata katika kipindi hiki kigumu cha kuenea duniani virusi hatari vya corona.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani kuondoka kwa fedheha madarakani, utawala huo umetekeleza hatua mpya ya kuvuruga juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kupambana na maradhi ya corona. Wizara ya Fedha ya nchi hiyo Jumatano iliongeza katika orodha yake ya vikwazo majina ya watu wawili na mashirika 16 ya Iran. Taasisi ya Haram ya Imam Ridha (as) na shirika lenye msingi wa elimu la Barakat, ambalo limetengeneza chanjo ya kwanza ya corona nchini, ni miongoni mwa taasisi na mashirika hayo yaliyoongezwa kwenye orodha hiyo ya vikwazo.

Serikali ya Trump katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, yaani tokea kuanza siasa za mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, haijawahi kuwa na mtazamo wa kibinadamu kuhusu taifa la Iran. Hivi sasa ikiwa inatekeleza siasa  hizo hizo zisizo ambazo hazijawahi kuwa na mafanikio yoyote ya maana dhidi ya Iran imeamua kuliwekea vikwazo shirika la kielimu, yaani Barakat, ambalo limefanya utafiti na kuwa na mchango mkubwa katika uwanja wa kutengenezwa chanjo ya kwanza ya corona nchini.

Tehran imetangaza mara nyingi kwamba Marekani imekuwa ikichukua hatua za upande mmoja na za kiuadui dhidi ya watu wa Iran na hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuenea corona duniani, ili kuwanyima uwezo wa kufikia dawa na vifaa vya afya na matibabu.

Kama alivyosema Jackie Northam ripota wa idhaa ya NPR, vikwazo vya Marekani vimetoa mashinikizo makubwa dhidi ya uchumi wa Iran na kudhuru mfumo wake wa huduma za afya na matibabu.

Suala hilo pia limeizuia Iran kununua chanjo za corona ambazo zimetengenezwa na baadhi ya nchi. Kwa kutilia maanani ukweli huo mchungu, Iran imeelekeza juhudi zake zote katika utengenezaji wa chanjo ya corona ndani ya nchi na tayari mashirika manane likiwemo la Barakat, yanafanya jitihada kubwa katika uwanja huo. Kuhusu hilo inaonekana kuwa watawala wa Washington wameshangazwa na kuchanganyikiwa kabisa kutokana na msimamo wa wazi wa hivi karibuni wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa kupiga marufuku uagizaji nchini chanjo za corona kutoka Marekani na Uingereza.

Msimao huo una maana ya kutiliwa shaka ubora na taathira ya chanjo ya corona iliyotengenezwa na shirika la Marekani la Pfizer. Ni kutokana na ukweli huo ndipo utawala wa Marekani ukachukua hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya shirika la Barakat ili kujaribu kuvuruga na kuzuia mafanikio yake katika uwanja wa kutengeneza chanjo ya Kiirani ya corona.

Tokea wakati wa kuanza kuenea corona nchini Iran nchi nyingi za dunia na hasa Russia, China na Venezuela zililitaka Shirika la Afya Duniani WHO, liishinikize Marekani ili ipungeze vikwazo vyake vya kidhalimu dhidi ya Iran kwa ajili ya kurahisisha uingizwaji nchini bidhaa muhimu kama vile dawa na vifaa vya afya kwa ajili ya kupambana na corona. Ombi hilo pia lilitolewa na washirika wa karibu wa Marekani barani Ulaya, lakini utawala wa Trump si tu kuwa umeyapuuza maombi hayo yote, bali katika miezi ya karibuni umekuwa ikiweka vikwazo vipya na kuzidisha vikwazo vyake hivyo vya kinyama kila wiki, dhidi ya watu wa Iran.

Kwa mujibu wa Elizabeth Rosenberg, afisa wa zamani wa ngazi za juu katika wizara ya fedha na mchambuzi mashuhuri wa masuala ya siasa wa Marekani, mashinikizo na vikwazo vya kiuchumi vya Marekai vinaonekana wazi hasa katika uwanja wa Iran kushindwa kununua vifaa vya matibabu na afya.

Kuendelea vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran sambamba na kuenea virusi vya corona, bila kujali masuala ya kiafya na kimatibabu, kumepelekea wengi kuamini kwamba 'mashinikizo ya juu kabisa' ya Marekani dhidi ya Iran yanahusisha pia masuala ya kibinadamu na mfumo mzima wa afya na matibabu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa maneno mengine ni kuwa, utawala wa Trump sasa unatekeleza 'ugaidi wa kimatibabu' sambamba na 'ugaidi wa kiuchumi' dhidi ya taifa la Iran na hivyo kuhusika kikamilifu na jinai za kibinadamu dhidi ya watu wa Iran.

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni