?>

Ulaya inajiua kwa kuiwekea Russia vikwazo vya nishati

Ulaya inajiua kwa kuiwekea Russia vikwazo vya nishati

Mataifa ya Ulaya yanajipiga risasi mguuni kwa kuweka vikwazo vya kuzuia ununuzi wa nishati kutoka Russia huku zikitii maamrisho ya Marekani.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Hayo yamesemwa na Igor Sechin, mkuu wa kampuni kubwa ya mafuta ya Russia ya Rosneft ambaye ameongeza kuwa, "Ulaya inajiua katika sekta ya nishati kwa kuiwekea Russia vikwazo."

Akizungumza katika Kongamano la Kiuchumi la Kimataifa la St. Petersburg (SPIEF), mkurugenzi wa Rosneft ameendelea kusema kuwa,  "Wao [nchi za Umoja wa Ulaya] wanapoteza utambulisho wao na nguvu zao za ushindani kwa Marekani."

Hapo awali, Rais wa Russia Vladimir Putin alivitaja vikwazo hivyo kuwa ni upanga wenye makali kuwili, akisema viongozi wa nchi za Magharibi wamesababisha uharibifu mkubwa kwa uchumi wa mataifa yao kwa kuweka vikwazo hivyo.

Putin aliongeza kuwa hasara ya moja kwa moja ya Umoja wa Ulaya kutokana na vikwazo inaweza kuzidi dola bilioni 400 kwa mwaka mmoja, na gharama hizo zitabebwa na raia wa umoja huo.

Putin aidha amesema ukoloni mamboleo ndio umesababisha migogoro wa kibinadamu inayoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali duniani; na kwamba Marekani na nchi za Ulaya ndizo zinazopaswa kubebeshwa dhima iwapo dunia itatumbukia kwenye baa la njaa.

Rais wa Russia amesisitiza kuwa, "ongezeko la bei ya mafuta duniani, mfumko wa bei za bidhaa, migogoro ya chakula, gesi na mafuta yote hayo yametokana na makosa ya kimfumo kwenye sera ya uchumi ya utawala wa sasa wa Marekani, na madola ya Ulaya."

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*